Mtunzi: Aisha Athumani    

 

 

Editing na kusaidia: Fransiska Maleko

Lengo la story

Lengo la story ni kuonyesha ushirikiano kati ya nchi na nchi na kuweza kutengeneza story ya lugha mbili tofauti ili iweze kusomwa na watu wa mataifa mawili. Story hii ni ya kuburudisha na kuonyesha utamaduni wa kitanzania ili kuona tofauti baadhi ya mambo.

 

 

Imeandaliwa mwaka 2013/ Tanzania/ Dar es Salaam.

A i s h a . a t h u m a n i @ h o t m a i l . c o m    

F r a n z i s k a . m u e l l e r _ @ h o t m a i l . d e

Haki zote zimehifaziwa.

 


Scene 1

Inaoneka familia yenye mama na watoto wawili. Mtoto wa kwanza Esha na wapili Shulea na mama yao akiwa kalala kwenye kiti anaumwa. Huku watoto wao wakiwa pembeni yake. Mama anawasimulia juu ya ugonjwa wake.

 

 

Mawazo

Anaonekana mama Esha akiwa ana mimba ya Shulea na akiwa kitandani anaumwa pembeni akiwa baba Esha wakiongea.

 

Baba Esha

Mke wangu tumeangaika sana hospital lakini wanasema siku za kujifunguwa bado na hauna tatizo lakini bado unaumwa.

 

Mama Esha

Lakini mume wangu hamna jinsi tumuombe tu mungu.

(Akikunja uso kwa maumivu.)

 

Baba Esha

Sawa ila mungu anasema jisaidie nikusaidie kwa hali hii tuna mtihani hata mtoto wetu Esha tunamtia unyonge. Dah! Yaani najuta kwa nini ulishika ujauzito.

 

Mama Esha

(Akiongea kwa unyonge.)

Usiseme hivo mume wangu.

 

Esha

(Akionekana akiingia ndani huku akiwa kavaa uniform za shule akitoka shule akiita.) Mama! Mama! Baba! Babaaaa!

 

Mama Esha

(Akimuangalia baba Esha usoni.)

Haya mtoto kaludi shule kampe chakula

 

Baba Esha

(Anaonekana akiinuka kwa unyonge na kuelekea sebureni alipo kuwepo Esha.)

 

Esha

(Akivua begi na kurusha kwenye kiti. Kasha anajirusha kwenye kiti na kukaa.)

Shikamoo baba.

 

Baba Esha

(Anamuangalia Esha huku akitabasamu.)

Vipi mamii!

 

 

Esha

Mama yupo wapi na wewe mbona hujaenda kazini?

 

Baba Esha

Mama yako katoka kidogo na sijaenda kwa sababu nikuandalie chakula.

 

Esha

(Akitabasamu)

Haya kanipe nile hapahapa.

 

 

Scene 2

Baba Esha na mama Esha wakiwa sebureni wamekaa kwenye kiti wanaongea.

 

Baba Esha

Mke wangu nimepata wazo. Mi naona siku zinaenda ugonjwa bado. Mi naona tuende kwa mganga tukajaribu tu.

 

Mama Esha

(Akiguna.)

Mmh! Mume wangu lakini……..

 

Baba Esha

Hakuna cha lakini.

(Akiinuka na kuelekea chumbani.)

 

Mama Esha

(Akiguna.)

Mmh!

 

 

Scene 3

Wanaonekana mama Esha na baba Esha wakiwa kwa mganga. Ndani ya kinyumba cha udongo na mabati ya makuti wamekaa chini mchangani. Kisha mganga anzakuongea nao.

 

Mganga

Hakuna cha kuongea ugonjwa nauwona ni mdogo sana kuutibu ila ukiuwacha ni mkubwa. Unaweza kukusababishia hata kutoa uhai wako.

 

Baba Esha

Kivipi?

 

Mganga

(akicheka kwa sauti akiliza manyanga.)

Nisikilizieni kwa umakini.

 

Baba Esha na mama Esha

(Wakiangaliana kwa mshangao.)

 

Mganga

Titizo mkeo alizaliwa kwa madawa kwa hizo yale madawa ndio yanampa tabu inabidi yapoozwe. Sasa tiba inabidi alete picha na ihifaziwe kwenye fremu ndo tuanze tiba.

 

Baba Esha

Sawa mganga.

 

Mganga

(Akiongea kwa sauti.)

Sema tawile mganga.

 

Baba Esha

(Kwa uwoga akiongea.)

Tawile tawile mganga.

(Anaonekana akimwinua mke wake na kuondoka.)

 

 

Scene 4

Baba Esha na mke wake wakiwa kwa mganga. Mama Esha anaonekana kafunikwa shuka. Anasikitika akikohoa kwa sauti.

 

Mganga

(Akimfunuwa shuka mama Esha.)

Haya inatosha sogea kwa huku.

(Akionyesha kwa kidole.)

Haya hii picha yako nimeiwekea dawa ili ikusaidie ugonjwa usikurudierudie ihifadhi vizuri ili isivunjike na mtu yeyote asije akaichukua. Muhiu iweke ndani kwako chumbani kwa hizo itunze ugonjwa usije ukarudi na hakikikisha inakuwepo ndani kwako na sio ukaiweke kwa mtu mwingine ikiwa mbali. Bado ugonjwa utakusumbuwa. Umenielewa?

 

Mama esha

(Akiitikia kwa unyonge.)

Tawile mganga

 

Mganga

Haya mnaweza kuondoka.

 

Baba Esha

(Anamuinua mke wake na kuondoka.)

 

 

Scene 5

Baada ya mwezi mmoja familia ya baba Esha ilibadilika. Mama Esha alijifungua mtoto wa kike ambaye jina lake ni Shulea. Baba Esha kazini kapandishwa cheo. Kasha wanaonekana baba Esha na mama Esha wakiwa wanajadiliana kuhusu mtoto wao Esha kwenda kusoma boding na jinsi gani ya kumpata mlinzi wa getini. Mara hodi inagongwa.

 

Mama Esha

(Anainuka kuelekea mlangoni kumuangalia mtu anaegonga. Mara anafungua mlango.)

Karibu pita ndani.

(Akinyoosha mkono kwa ishala apite ndani.)

 

Mgeni

(Anaonekana akiingia ndani na kukaa kwenye kiti.)

 

Mama Esha

(Akikaa kwenye kiti huku akimwangalia baba Esha usoni na kuongea.)

Mmmh! Mume wangu ebu msikilize.

 

Baba Esha

Na wewe mke wangu mbona hujiami? Sio nimsikilize sema tumsikilize.

 

Mgeni

(Anaonekana akiwa mnyonge.)

 

Mama Esha

Mh! Mume wangu na wewe naye. (huku akitabasamu)

 

Mgeni

(Akimwangalia mama Esha usoni na baba Esha huku akiwa na udhuni)

Mimi nilikuwa na shida ya kazi.

 

Baba Esha na mama Esha

(Wakiangaliana usoni kwa mshangao kasha wanaongea kwa pamoja.)

Sawa lakini utakuwa getini.

 

Mgeni

(Akiongea kwa unyonge.)

Sawa nashukuru.

 

Baba Esha

(Akimwangalia usoni mgeni.)

Kwanza unaitwa nani?

 

Mgeni

(Akionekana akijifikiria kidogo na kuongea kwa kigugumizi.)

Naitwa… naitwa Chidi ukipenda Rashidi.

 

Mama Esha na baba Esha

(Wanaonekana wakiongea huku wanatabasamu na kuongea kwa pamoja.)

Tutakuita Chidi.

 

Wote

(Wanacheka)

 

 

Scene 6

Anaonekana Shulea akiwa kalala kwenye kiti sebureni na mama Esha anaandaa vitu vya Esha vya shuleni anapokwenda kusoma Mwanza. Mara baba Esha anaingia ndani kwa ajili ya kumsafirisha Esha.

 

Baba Esha

(Akikaa kwenye kiti na kucheza na Shulea.)

Mh! Mama watoto tayari kila kitu?

 

Mama Esha

(Akiacha kazi aliyokuwa anafanya na kuongea na mumewe huku akimuangalia usoni.)

Sasa mume wangu hapa mpaka Ubungo unaenda na gari yako halafu mnapanda gari nyingine hafu hii gali yetu atairudisha nani nyumbani?

 

Baba Esha

Inabidii nikodi teksi mpaka Ubungo ungekuwa unajua kuendesha ungetupeleka wewe.

 

Mama Esha

(akitabasamu)

Na wewe usinishushue. Haya kila kitu tayari. Mpigie simu mwenye teksi aje awapeleke maana…

 

Baba Esha

(Anaonekana akibonyeza simu.)

Haya tena na huyo Esha mwenyewe yupo wapi?

 

Mama Esha

Yupo ndani kwake.

(Akiita kwa sauti.)


 

Intercut

Anaonekana mlinzi chidi akiwa anawaza huku akiongea.

 

Chidi

Nina uhakika huyu ni chaguo langu hata kama ana mume na watoto. Mimi sijali. Yaani mpaka nimeweza kujigeuza mlinzi. Napata tabu wakati sina tabu wala shida.

(Ghafla anashtushwa na honi ya gari iliokua ikilia getini. Anafungua geti.)

 

Dereva wa teksi

(Akishusha kioo cha gari.)

Vipi ndugu umelala au? Tuachane na hayo mzee yupo ndani?

 

Chidi

Ngoja nikakuitie.

(Anaonakana akielekea ndani na kumwambia Baba esha kuwa dereva kaja.)

 

Baba Esha

(Akionekana akishangaa.)

Khe! Makubwa nisiwasindikize mwanangu. Simwoni mpaka likizo. Nataka nichezecheze naye njiani.

 

Baba Esha

(Akimwangalia usoni mke wake.)

Najua ila utamsumbua mtoto na magari.

 

Mama Esha

(Akiguna)

Mh! Sawa safari njema.

(Akimbusu Esha. Kasha anawasaidia kutoa mizigo nje na kuingiza kwenye gari.)

 

                                                                Mlinzi Chidi

(Anaonekana akifungua geti na kuruhusu gari la baba Esha kuondoka.)

 

Baba Esha

(Anaonekana akiwasha gari na kupunga mkono kwa mkewe na mlinzi na kuondoka.)

 

 

Intercut

Mama Esha anaonekana kumuamrisha Chidi kufunga geti.

 

Mama Esha

We! Chidi mbona umesimama baada ya kufunga geti?

(Anaonekana anaelekea ndani.)

 

 

 

Chidi

(Akifunga geti huku akimwangalia Mama Esha.)

Dah! Mama samahani ila nisubiri nina maongezi na wewe.

(Akifunga geti na kuelekea kwa Mama Esha.)

 

Mama Esha

(Anaonekana kasimama baradhani karibu na mlango wa kuingia ndani na kumwangalia Chidi.)

Umesemaje?

 

Chidi

(Akielekea kwa mama Esha na kusimama.)

Mama ulijisikiaje Baba alivyoondoka?

(Akimwangalia huku akikunja sura.)

Hivi wewe una akili. Mimi najisikiaje. Wewe! Inakuhusu nini?

 

Chidi

(Akionesha hudhuni huku akiongea.)

Samahani mama nimekuhuliza tu kwa sababu naona umezoeana na baba sana.

 

Mama Esha

(Akimnyoshea kidole.)

Wewe sipendi unipande kichwani maana siku hizi nakuona mambo mengine hayakuhusu.

(Anamsonya na kuingia ndani.)

 

Chidi

Anamwangalia mama Esha na kujipiga piga kichwani kasha anaelekea sehemu yake ya kukaa nakujiinamia kwa mawazo.

 

 

Scene 7

Anaonekana Chidi akiingia sebureni huku Shulea akiwa amelala katika kiti. Chidi anafika na kumnyanyia na kumpakata. Mara mama Esha anatokea na kumkuta Chidi amempakata Shulea.

 

Mama Esha

(akishangaa)

Wewe!! Mbona uko huku?

(Akishika kiuno huku akishangaa.)

 

Chidi

(Akimwangalia.)

Samahani mama. Nilikuwa nataka kukuomba kitu.

 


 

Mama Esha

(Anashangaa.)

Kuniomba kitu? Kitu gani? Hebu sema.

 

Chidi

Samahani mama nilikuwa naomba ruhusa niende nikanunune nguo kesho na hela yangu ulionipa mwezi huu.

 

Mama Esha

(Akitabasamu.)

Sawa ila usichelewe siunajua geti litakuwa halina mtu.

 

Chidi

(Akimwangalia mama Esha huku akitabasamu.)

Asante sana sitachelewa.

 

Mama Esha

(Anaelekea katika kiti na kukaa.)

Haya kaendelee na kazi.

 

 

Scene 8

Chidi anaonekana akiwa nyumbani kwake huku akiwa na rafiki zake watatu wakiongea sebureni.

 

Rafiki wa Chidi

(Akiongea kwa dharau.)

Hivi Chidi maisha hayo sio unatutia aibu?

 

Chidi

(Akimwangalia usoni.)

Kilicho nileta sio hiko. Ni biashara zangu zinaendaje na kuangalia nyumba yangu.

 

Rafiki 2

Sio hivo Chidi. Tuna haki ya kukuambia hata kama bosi wetu.

 

Chidi

(Akikunja sura.)

Jamani!! Nimewaambia yule mwanamke nampenda na ndio maana nafanya hivi nikishampata basi hali hii itaisha.

 


 

Rafiki 3

(Akiwaangalia wote.)

Kwani jamani huyu mwanamke alimwona wapi? Na ana nini mpaka hali hii imejitokeza? Mtu ana pesa zake ana biashara zake. Anashindwa kusimamia eti. Mwanamke isitoshe nasikia ana watoto na mume wake.

 

Rafiki 2

Sikiliza niwaambie kuhusu huyu mwanamke.

 

 

Flashback

Wanaonekana baba Esha na mke wake wakiwa wamepaki gari pembeni ya duka la nguo za watoto. Huku Chidi na rafiki 2 wakiwa wanaingia kwenye gari yao. Ghafla Chidi anamwona mama Esha wakishuka kwenye gari na kuelekea kwenye duka la nguo.

 

Chidi

(Anapoingia kwenye gari na kuegemea skanio.)

 

Rafiki 2

(Anaingia kwenye gari na kukaa kwenye kiti na kumshangaa Chidi.)

Oya!! Vipi mkuu? Mbona hivyo?

 

Chidi

(Akiinua shingo na kumwangalia rafiki yake.)

Dah! We acha. Hebu mwangalie yule mwanamke. Kiukweli nimetokea kumpenda.

 

Rafiki 2

(Akishangaa)

We! Mbona maajabu? Siunamwona yupo na mumewe. Tena nadhani wana mtoto. Si unaona wanapenda kununua nguo za watoto?

 

Chidi

(Akikunja sura.)

Hivyo vyote haunihusu nimekuambia nimetokea kumpenda.

 

Rafiki 2

(Akishusha pumzi)

Dah! Poa

(Akifungua mlango wa gari.)

 

 


 

Intercut

Mama Esha na Baba Esha wanaonekana wakitoka dukani na kuelekea kwenye gari lao na kuondoka. Huko Chidi anampa nauli rafiki yake amtangulie nyumbani na yeye anawafatilia wakina mama Esha nyumbani kwao. Mama Esha anapofika nyumbani kwao Chidi anageuza na kurudi kwake.

 

 

Scence 8

Chidi akiwa nyumbani kwake anaongea na rafiki wake wawili akiwa amekaa sebureni.

 

Chidi

(Akimuangalia Rafiki 2 usoni.)

Yaani hata sijui kwa nini imenitokea vile jana yaani mpaka sasa sielewi. Kiukweli yule nitahakikisha anakuwa mke wangu mimi.

 

Rafiki 2

(Anasikitika.)

Sidhani utampata.

 

Chidi

(Akitabasamu na kuongea.)

Nipe wiki moja uone.

 

Rafiki 2

(Akicheka kwa sauti na kuinuka.)

Yaani ushindwe kuangalia mambo yako umfikirie yule mzazi hata harufu ya maziwa haijamisha.

(Anaelekea kwenye friji na kumimina maji kwenye glasi.)

 

Chidi

Yawe maziwa yawe togwa habari ndio hio.

(Akiinuka na kuelekea chumbani kwake.)

 

Rafiki 2

(Akimuangalia Chidi huko akinwa maji.)

 

 

Intercut

Rafiki 2 akiwa anapomaliza kuwasimulia Chidi anainuka kwa hasira.

 

Rafiki 3

Dah! Mkubwa si ukae kwanza tukupe ushauri.

 

Wote

Wanaangaliana kisha Chidi anaondoka.

 

Scene 9

Chidi anaonekana akiwa anafungulia geti na kuliruhusu gari liingie. Mara anashuka baba Esha. Gari linageuza kisha baba Esha anatoa simu nakumpigia mama Esha.

 

Mama Esha

(Akiwa Akitokea chumbani na kuelekea sebureni mara simu yake inaita. Anasimama nakupokea.)

Halo! Vipi mume wangu?

 

Baba Esha

Hm. Sasa kuna mtu nimemtuma hapo nyumbani. Kasema kafika ila sasa toka nje ukamsikilize.

 

Mama Esha

Haya ngoja niende.

(Anakata simu nakurusha kwenye kiti kisha kuelekea nje.)

 

Baba Esha

(Akimuangalia mke wake na kumtabasamu kwa furaha.)

 

Mama Esha

(Akishangaa na kushusha pumzi.)

Jamani mumue wangu. Unaweza kuniua! Ndo nini kunishtukiza?

(Akimfuata na kumkumbatia.)

 

Baba Esha

(Anambusu mke wake na kuelekea ndani huku Chidi anawaangalia kwa uwifu.)

 

Mama Esha

(Akitabasamu nakumfuata mumewe.)

 

Chidi

(Anaonekana akiwa na mawazo kwa kitendo kilichotokea. Usoni akiwa na hasira.)

 

 

Baada ya miaka saba

Mama Esha akiwa na Shulea wakiwa wanaelekea Shoprite kununua vitu vya ndani. Wakiwa wanafungua mlango wa gari mara mtu anakuja na kuleta taarifa ya msiba. Kuwa Baba Esha kafariki kwa ajali. Shulea alianza kupiga kelele na kulia na Mama Esha anazimia.

 

Chidi

(Akiwa na wasiwasi na kuchanganikiwa.)

Mungu wangu!

(Anainama na kuchukua simu ya Mama Esha na watu kuwataarifu ya msiba.)

Mama Esha

(Anaonekana anazinduka na watu wamejaa na kuanza kulia na kuongea.)

Esha Mama haujamwona Baba yako kwa muda mrefu sasa uje uone maiti basi.

 

Watu msibani

(Wananagaliana na kuanza kujadili kwa msikitiko.)

 

Ndugu wa marehemu

Jaamani tusikilizane Maiti yetu tutaizika leo halafu mtoto wake wa kwanza hatutampa taarifa kwa sababu karibia anamaliza mtihani wa form four. Kwa hio tunaweza tukamsababishia kafeli. Wanandugo wote tulijue suala hilo kwamba tusimpe taarifa Esha. Haya, baada ya hayo tuinuke na tuelekee makaburini.

 

Mama Esha

(Akiinuliwa huko analia.)

 

Shulea

(Akilia)

Baba? Uko wapi Baba? Baba…. Baabaaaaaa uko wapi sasa???

 

 

Baada ya mwezi mmoja

 

Rafiki wa Esha

(Akionekana anabisha hodi na Chidi akifungua mlango na kuingia ndani.)

 

Chidi

Kuna tatizo gani?

 

Rafiki wa Esha

Sina tatizo bali nimekuja kwa rafiki yangu.

 

Chidi

We mtoto! Tangia nimeanza kazi sijawahi kusikia marafiki wakiingia humu ndani.

 

Rafiki wa Esha

We vipi? Basi niitie mwenyeji.

 

Chidi

Haya subiri sasa.

(Akimwita Shulea na anatoka nje.)

 

Shulea

(Akitabasamu.)

We mjomba Chidi! Mruhusu aje! We vipi? Jamani dada karibu upite ndani.

(Akimwita Mama yake na Mama anatoka na kukaa sebureni.)

 

Rafiki wa Esha

(Akikaa kwenye kiti.)

Shikamoo Mama.

 

Mama Esha

Marahaba mwanangu. Za shule?

 

Rafiki wa Esha

Nzuri tu. Mitihani tumemaliza. Vipi Esha yupo wapi?

 

Mama Esha

Hm. Esha kasema atarudi wiki ijao. Si unajua rafiki yako alivyo mzito hayupo shapu.

 

Rafiki wa Esha

Na kweli Mama ila nilimwacha shule akasema anarudi kesho kutwa. Nashangaa tena wiki ijayo.

 

Mama Esha

Ah! Hata hivyo mwache kwanza apumzishe akili huko. Maana…

 

Rafiki wa Esha

Kwa nini tena? Mbona unasema hivyo?

 

Mama Esha

Ah! Hamna kitu. Sasa mwanangu mi nipo ndani napumzika siupo na Shulea hapo?

 

Rafiki wa Esha

Hata hivyo naomba niende naye Shulea beach.

 

Mama Esha

(Akiinuka na kuelekea ndani.) Sawa kuweni makini na msichelewe kurudi.

 

Rafiki wa Esha

Shulea kajiandae basi au?

 

Shulea

(Akiwa na uso wa furaha.)

Ngoja nikaanadae hakuna cha au!

 

 

Scene 10

Chidi anaonekana sebureni akimwita Mama Esha. Mara Mama Esha anaitika sauti inatokea chumbani.

 

Chidi

(Akimfuata chumbani. Huku akijiweka vizuri.)

Basi kumbe uko chumbani. (Anaingia chumbani na kukaa kitandaani.)

Mama Esha

(Akishangaa.)

We vipi? Una nini?

 

Chidi

(Akimuangalia usoni kwa huruma na kwa kumtamani.)

Kwanza samahani kwa kuingia chumbani kwako leo ila kiukweli uvumilifu umenishinda. Ukweli ni kwamba mimi sina hazi kwa kuwa mlinzi wa getini. Nimekuwa mlinzi kwa sababu yako.

 

Mama Esha

(Akimuangalia kwa hasira na mshangao.)

Kwaani kuna siku nilikuambia kuwa acha kazi?

 

Chidi

Sio hivyo ila nimekuja kufanya kazi kwa sababu nakupenda. Tangia nilivyokuona kwa mara ya kwanza barabarani ukiwa wewe na mumewe na mtoto wenu. Ila tuachane na Yote. Hii nafasi ni yangu sasa.

 

Mama Esha

(Akimuangalia kwa hasira.)

Hivi we unataka kazi au?

 

Chidi

(Akimwangalia kwa tamani.)

Mimi sina shida na kazi labda mwanao huyo anaye kuja akiwa ansubiri majibu ya mtihani wake. Akafanye kwenye ofisi yangu moja. (Akitabasamu.)

 

Mama Esha

Naomba toka.

 

Chidi

(Akimsogelea Mama Esha na kumshika.)

 

Mama Esha

Hebu niache. Nafasi hii ilikuwa na mume wangu tu basi.

 

Chidi

                                                               (Akitabasamu.)

Sasa si kafa?

 

Mama Esha

Kafa mwili. Kiakili nipo naye.

 

Chidi

(Akiendelea kumsogelea.)

Hebu achananaye aliyekufa.

 

Mama Esha

(Akishangaa maneno ya Chidi.)

Yaani siku aliyegongwa mume wangu ungekuwa haupo ningesema wewe umemua. Maana hayo maneno yako.

 

Chidi

(Akitabasamu.)

Kwaani kuua kitu gani na haswa ukipenda?

 

Mama Esha

Naomba ondoka. Nimesema ondoka. Na tena nisikuone eneo la nyumba hii kabla sijapiga simu polisi.

 

Chidi

Siwezi kuondoka kwaani nimepoteza muda kwa miaka mingi kwa ajili yako kwa kujua lazima utakuwa mke wangu.

 

Mama Esha

(Akichukua simu mezani na kubonyeza namba.)

 

Chidi

(Akimzuwia mkono asibonyeze simu.)

 

Mama Esha

(Kwa sauti.)

Niache!!! Nimesema niache!

 

Chidi

Naomba unisikilize. Naondoka ila…

(Akifuata picha ya mama Esha na kuitoa juu na kuondoka nayo kwa kasi na hasira na kuongea.)

Hii ndo kumbukumbu yangu kwako.

 

Mama Esha

(Akimkimbilia huko akilia.)

Chidi! Chidi njoo! Njoo Chidi, nimekubali! Chidi! Chidiiiiiiiiiiiiiiiiiiii… Chiiiiiiiiiiiiii… Chiiiiiiiiiiiiiii…

 

Chidi

(Anatoka nje ya geti kisha anasimamisha pikipiki na kuondoka.)

 

Mama Esha

(Analia.)

 

 

 


 

Scene 11

Anaonekana Mama Esha akiwa anamwaga Shulea kuwa awe makini na nyumba. Yeye hamwambii anapoelekea. Kwaani mambo yote hajawahi kumwambia Shulea.

 

Shulea

(Akimuangalia usoni mamake.)

Kwaani unaenda wapi?

 

Mama Esha

Wewe nimekuambia kuwa makini na nyumba na wala usitoke. (Anafunga mlango na kuondoka.)

 

Shulea

(Akimwangalia mamake kisha anajitupa kwenye kiti.)

 

 

Intercut

Anaonekana Mama Esha akiwa kachanganikiwa. Anaambiwa mganga kafa. Na pale kwa mganga wanakaa ndugu wa mganga.

 

Mama Esha

Jamani ni kweli?

 

Ndugu 1

Hatuwezi kudanganya ila na ninyi magonjwa ndio walivyo mkifanikiwa mnajisahau mpaka mpate matatizo. Ndo mnarudi. Sasa mganga tangia amefariki anamiezi sita. (Anaingia ndani.)

 

Mama Esha

(Akiondoka kwa unjonge.)

 

 

Intercut

Anaonekana Mama Esha anamalizia kuwasimulia wanawe juu ya ugonjwa anaumwa.

 

Esha

(Akimuangalia mamake kwa huruma.)

Mama usijali utapona. Ila ukimwona huyu Chidi utamjua?

 

Mama Esha

(Akiongea kwa tabu.)

Nitamjua tena kwa kuthibitisha. Nitachukua picha yake na kulinganisha na yeye. Lakini nina uhakika nitamjua.

 


 

Esha

Hio picha iko wapi?

 

Mama Esha

Kwenye dressing table ukifungua draw ya pili.

 

Esha

Basi ngoja mama nikachukue chakula ule angalau kidogo. (Anainuka na kuelekea jikoni.)

 

 

Scene 12

Anaonekana Esha akiingia kwa marafiki yake mara mlangoni anapishana na Chidi. Esha anaingia ndani na Chidi anatoka.

 

Esha

Shikamoo.

 

Chidi

(Akimwangalia Esha.)

Marahaba binti. (Akielekea safari yake.)

 

Esha

(Akiingia ndani na kukutana na rafiki yake. Akiwa akakaa sebureni kwenye kiti.)

 

Rafiki wa Esha

(Akimwangalia Esha kwa tabasamu.)

Eh he. Vipi besti? Karibu.

 

Esha

(Akikaa kwenye kiti.)

 

Rafiki

(Akimuangalia usoni Esha na kumshangaa.)

Vipi Esha una nini? Halafu nikuambie siumekutana na mjomba wangu? Yaani besti unisaidie anatafuta msichana wa kazi kama ukisikia huko mtaani kwenu. Yaani mjomba wangu anayo shida.

 

Esha

Haya mpaka nisikie. Vipi mama mdogo yuko wapi?

 

Rafiki wa Esha

Katoka. Na wewe vipi mama?

 

Esha

Yaani we acha. Kila siku nachanganikiwa.

 

Rafiki wa Esha

(Akimuangalia Esha usoni kwa huruma.)

Usijali naamini atapona.

 

Wote

(Wanakumbatiana.)

 

 

Scene 13

Esha na Shulea wakiwa chumbani. Esha akiwa kitandaani huko akishika picha ya Chidi. Na Shulea akiwa anabadilisha nguo anajiandaa kulala.

 

Esha

(Akimwangalia Shuea huko akiwa akashika picha.)

Hivi Shulea ukiangalia hii picha unaamini nini?

 

Shulea

Naamini kama huyu ndiye alichukua picha ya mama ambayo imesababishia tatizo mpaka leo.

 

Esha

Kingine?

 

Shulea

Hm. Sina kingine.

 

Esha

Mimi naamini pia huyu ndiye alimwua baba.

 

Shulea

(Akishtuka na kumangalia Esha.)

We Esha una uhakika gani? Maelezo Baba alipata ajali na tena yule alikuwa nyumbani.

(Akipanda kitandaani.)

 

Esha

(Akijifunika na kugeukia upande wa pili wa kitanda.)

Haya lakini jua kwenye pesa sio mwenzako. (Akilala.)

 

 

Scene 14

Esha akiwa anamsindikiza rafiki yake walipofika mbali kidogo. Na Rafiki wa Esha anaona mjomba wake ambaye ni Chidi. Rafiki anashtuka na kuomba msaada kwa Esha.

 

Esha

(Akishangaa na kutabasamu.)

Mjomba kafanyaje?

Rafiki wa Esha

Akiniona sijui itakuwaje. Nisaidie asinione. Yule kule anakuja hukohuko.

 

Esha

(Akimwonyesha chochoro aende.)

Sasa wewe. Ingia kule halafu mimi nitamzuga hapa hapa. Nitachezea simu ili nijue kafika wapi halafu nikushtue uende zako. Na mimi narudi nyumbani.

 

Rafiki wa Esha

Poa basi. (Akielekea kwenye chochoro haraka.)

 

 

Intercut

Mara mama Esha anashtuka anapomwona Chidi anakumbuka ile picha na kuanza kumwangalia kwa umakini. Chidi anapita haraka.

 

Rafiki

(Anafika kwa Esha na kuanza kucheka. Huko Esha akiwa na hasira.)

Yaani we acha angeniona ningekoma. Hapendi nizurule na ndo maana wazazi wangu walivyokufa sikutaka kukaa kwake na sipendi kwenda kwake maana mkali mpaka anakera. We ulimsalimia au ilikuwaje alivyopita?

 

Esha

(Akiwa serious.)

Sasa ngoja nimuwahi mama.

 

Rafiki wa Esha

(Akiwa anamwangalia usoni Esha na kushangaa.)

Vipi Wewe? Mbona hivyo?

 

Esha

Poa basi msalimie mamdogo.

 

Rafiki wa Esha

(Akiguna.)

Hm… Haya take care.

(Wanaonekana wote wawili wakiondoka.)

 

 

Scene 15

Esha na Shulea wanaonekana wakiongea sebureni.

 

Esha

Shulea kuna kitu nataka nikifanye ambacho mama kitamsaidia kupona.

 


 

Shulea

(Akimwangalia Esha kwa kejeli.)

Ufanye nini wewe?

 

Esha

Nakuambiaje? Hesabia mama atapona.

 

Shulea

We Esha! Cha msingi tumlee mama mpaka mungu atakapopenda hamna tena tiba ya mama.

(Akigeukea pembeni.)

 

Esha

Sasa ndo mungu kapenda Mama apone. Mtahakikisha mama anapona na atapona naamini.

 

Shulea

Niaaminishe tu lakini sina imani hio.

 

 

Scene 17

Anaonekana Esha kwa Rafiki yake na mamdogo wa rafiki yake anaonekana akiondoka.

 

Mama Mdogo

Jamani mi natoka. Vipi Esha lakini? Mzima?

 

Esha

Mi mzima Mama.

 

Mama mdogo

Umefika na mwenjeji natoka ila usijali. Jisikie upo nyumbani. Ila rafiki yako si upo naye. Mi sina dili saaaana.

 

Wote

Wakicheka na mamdogo akiondoka.

 

Esha

(Akiwa anakaa vizuri na kuanza kuongea.)

Hm…. Besti nina shida.

 

Rafiki

(Akimuangalia kwa umakini.)

Shida? Shida gani tena?

 

Esha

Mbona unaogopa?

(Akitabasamu.)

Rafiki

Hm… Ongea.

 

Esha

Unajua kwa sasa hela za benki zinaisha na hatuingizi pesa yoyote. Nyumbani kwetu hamna anayefanya kazi. Nimeona bora nifanye kazi ili niweze kusaidia angalau kidogo.

 

Rafiki

Hm…. Ndugu yangu utafanya kazi gani na hio form four? Au umesikia kazi?

 

Esha

Najua kazi ngumu. Ndio maana nataka msaada wako.

 

Rafiki

Mimi nikusaidie nini? Na ikiwa mimi na wewe wote tupo sawa.

 

Esha

Nataka kufanya ile kazi ya mjomba wako ulioniambia. Au kapata msichana wa kazi?

 

Rafiki

Eh… Esha ndo hapa umejishusha kabisa mwenzangu.

 

Esha

Jamani nimeamua kama hutaki kunionganisha niambie.

 

Rafiki

Hata kama siwezi kuona umeishiwa kiasi hicho. Kama ndo hivyo ni bora kuongea na mamdogo akutaftie kazi mjini lakini sio kazi ya ndani.

 

Esha

(Akionyesha kukasirika.)

Mimi nimeamua mwenyewe kufanya kazi za ndani na kama hutaki basi!

(Anainuka na kuondoka.)

 

Rafiki

(Akimuangalia.)

 

 

Intercut

Anaonekana Esha akiingia ndani kwao kwa hasira na kumpita Esha akiwa sebureni. Esha anaelekea chumbani na kujitupa kitandani. Kisha anainuka na kuchukua picha na kuangalia picha ya Chidi. Na rafiki yake anaonekana akiingia chumbani na kulala kitandani. Anaamua kumpigia simu Esha.

 


 

Shulea

(Akimfuata Esha chumbani akiwa na mshangao.)

Kwaani una nini wewe?

(Mara simu ya Esha inaita.)

 

Esha

(Anaiweka picha kitandani na kuchuka simu iliokuwa kitandani na kupokea.)

Unasemaje?

 

Rafiki wa Esha

Acha na hayo mambo.

 

Esha

Acha na mimi.

 

Rafiki wa Esha

Jamani Esha kama umeamua kufnaya kazi hio nitakuelekeza kwa mjomba.

 

Esha

(Akionekana sura kubadilika na kuwa nyenye furaha.)

Asante rafiki yangu mimi nimeamua kufanya hio kazi.

 

Rafiki

Lakini mimi siunajua nitakua nakuelekeza lakini mimi siendi. Siunajua mi na mjomba hatuelewani nitakuelekeza tu.

 

Esha

Usijali nielekeze tu. Nitafika.

 

Rafiki

Poa.

 

Esha

Poa wangu. (Anakata simu na kukaa kitandani. Huko akitabasamu.)

 

Shulea

(Akimwangalia.)

Unaweza kudata. (Anafungua mlango na kuelekea sebureni.)

 

 


 

Scene 16

Esha akionekana akiwa anongea na Shulea.

 

Esha

Shulea naomba kitu kutoka kwako.

 

Shulea

Ongea tu. Kitu gani?

 

Esha

Mimi nataka ufight na mama anapona.

 

Shulea

Esha ndugu yangu dada yangu. Wapi unaenda na unarudi lini? Na mama je?

 

Esha

Ndo hicho kitu nataka unisaidie kwamba mama akiniulizia umwambie nimepata kazi. Naingia asubuhi sana natoka usiku sana.

 

Shulea

Kwaani unakwenda wapi?

 

Esha

Kuna mtu nimeongea naye kasema atanisaidia kumtibu mama. Ila mimi niwepo mpaka dawa ikamilike ndo nimletee mama.

 

Shulea

Una uhakika naye?

 

Esha

Nataka Mama yangu apone. Kwaani sijamfaidi nikiwa na akili zangu.

 

Shulea

Haya mimi nitabaki na mama ila kuwa makini siunajua unaniacha na mama.

 

 

Scene 17

Anaonekana Esha akigonga mlango kwa Chidi. Mara Chidi anafungua mlango na kukutana uso kwa uso na Esha.

 

Esha

Shikamoo.

 

Chidi

Marahaba. Nikusaidie nini binti?

 

Esha

(Akimwangalia usoni kwa uoga.)

Samahani.

 

Chidi

(Akiwa anakunja uso.)

Bila ya samahani. Kwaani nikusaidie nini?

 

Esha

Nilikuwa nina shida ya kazi.

 

Chidi

Hm… Kazi gani?

 

Ehsa

Hata za ndani.

 

Chidi

                                                  (Akionekana akifikiria kidogo.)

Hm... Hm… Ok karibu ndani Hm…

 

Wote

Wanaonekana wakiingia ndani na kukaa kwenye kiti huko wakiongea.

 

Chidi

(Akimwangalia usoni Esha kwa sura ya kawaida.)

Ehe. Unaitwa nani?

 

Esha

(Kwa wasiwasi.)

Naitwa Fransiska.

 

Chidi

(Kwa mshangao.)

Unaitwa Fransiska?

 

Esha

Ndio naitwa Fransiska.

 

Chidi

Basi mimi nitakuita Fransi.

(Mara Chidi anamwita mwanawe na mdogo wake ili waje awatambulishe. Mara wanaonekana wamefika.)

 

Chidi

(Anamuangalia mdogo wake usoni ambaye jina lake Ally.)

Ally, huyu jina lake Fransiska atakwepo hapo nyumbani kwa ajili ya kazi za ndani.

 

Ally

(Akimwanglia Esha usoni.)

Hm… Unakaa wapi kwani?

 

Esha

(Akiwa na kigugumizi akiwa anaongea.)

Mimi Mimi Mimi natokea kijiji fulani kinaitwa matombo.

 

Ally

(Akitabasamu.)

Hm… Hiki kijiji noma. Karibu. Mengi tutakuwa tunaongea wewe si upo? Halafu nisisahau kaka Chidi mbona haumtambulishi mwanao?

 

Chidi

Ah! Kweli huyu ni mwanangu anaitwa Rama.

 

Esha

Haya asante kwa kuwafahamu.

 

 

Intercut

Anaonekana Shulea akiwa na Mamake akimlisha uji.

 

Mama

(Akiugulia.)

Ah…. Uh… Yala…

 

Shulea

(Akiwa na udhuni huko machozi yanamtoka.)

Usijali mama yangu utapona usijali mama.

 

Mama

Hm…

 

Shulea

Basi Mama jitahidi huo uji mama yangu.

 

 

Scene 18

Asubuhi

Anaonekana Esha akiwa anafagia mara Chidi anatokea na kuongea na Esha.

 

Chidi

He Fransi nimesahau kukuambia chumbani kwangu ni marufuku kwa mtu yeyote kuingia. Sawa?

 

Esha

(Akionekana kustuka na kunyongonyea.)

Sasa nikitaka kufanya usafi?

 

Chidi

Usafi wa chumbani kwangu nafanya mwenyewe sitaki mtu yeyote kuingiza.

 

Esha

(Akiitikia kwa unyonge.)

Sawa Kaka sitoingia.

 

Chidi

Haya endelea na kazi zako. (Akionekana kuelekea chumbani kwake.)

 

Esha

(Akiwa kaacha fagio chini huko anafikilia.)

Sasa itakuwaje chumbani kwake hamna kuingia mtu. Ina maana mama yangu hatopona. Hm! Haiwezekani! (Anachukua fagio na kuendeleza kufagia.)

 

 

Intercut

Chidi

(Akiwa Chumbani kwake akiwaza.)

Bora nilivyomwambia Fransi maana ningechelewa angeingia ndani na angeona hii biashara yangu ya madawa ya kulevia.

 

Scene 19

Anaonekana Shulea kalala kwenye kiti sebureni anaangalia TV akionenkana kunogewa na kipindi cha TV.

 

 

Intercut

Wanaonekana Esha Ally na Rama wakiwa mezani wakinywa chai. Huko Rama anakunywa chai huko akiwa anaimba.

 

Rama

(Akiimba.)

Dada huyo anaolewa. Dada huyo anaolewa. Mali kashatolewa. Mali kashatolewa. Dada huyo…

 

Ally

Ha Rama! Unamchokosha Fransi!

 

Esha

We mwache nimeshamjua hanichokozi.

Rama

Aka mi sinaimba tu.

 

Esha

Haya endelea kuimba. Kwani si tumesemaje?

 

 

Scene 20

Usiku

Esha anaonekana akiwa kitandaani huko anamwazia mama yake. Machozi yakimtoka. Mara anapitiwa na usingizi mpaka asubuhi. Na Chidi anamgongea mlango.

 

Chidi

(Akigonga.)

We Fransi! We Fransi!

 

Esha

(Akishtuka na kueleka kufungua.)

Shikamoo kaka.

 

Chidi

(Akiwa na hasira.)

Marahaba. Sasa hivi saa ngapi?? Rama hajakunwa chai ili aende shule. Wewe umelala. Naona kazi umechoka.

 

Esha

(Akiwa na hofu.)

Hapana kaka nimepitiwa tu na usingizi sijachoka kazi.

 

Chidi

(Akiondoka kwa hasira na kuelekea kwenye biashara zake.)

 

Esha

(Anaonekana ana hofu na kurudi chumbani kwake na kuvaa haraka haraka. Na kwenda kuandaa chai na kufanya usafi)

 

 

Scene 21

 

Nyumbani kwa kina Shulea jioni

Mama Shulea anaonekana akiwa amekaa chini kamegemea Shulea huko akilia.

 

Shulea

(Akimuangalia usoni mama yake.)

Mama, sasa unavyoachaga kula ugonjwa ndo unazidi. Mimi sielewi. Nazidi kuchanganikiwa. Na nahisi dunia imenielemea.

Mama Esha

(Akiugulia na kuongea kwa sauti ya unyonge.)

Mwanangu sio nakataa ila sisikii hamu ya kula kabisa.

 

Shulea

Ndio, mama najua ila jitahidi angalau kidogo. (Akimlisha.)

 

 

Scene 22

 

Rafiki wa Esha

(Anaonekana kwa kina Esha na kumkuta Shulea kakaa nje akichezea simu yake.)

 

Shulea

(Akiwa kakaa kwenye kiti akiwa anacheza simu yake huko akitabasamu.)

 

Rafiki wa Esha

(Akionga geti.)

Hodi hodiiiii.

 

Shulea

(Akiangalia getini kwa kutaka kujua nani anagonga mlango.)

Fungua tu. Geti liko wazi.

 

Rafiki wa Esha

(Akiingia kwa furaha.)

Hm! Shulea kwa raha zako maana ilo pozi.

 

Shulea

(Akitabasamu huko akimwangalia Rafiki.)

Nina raha gani mwenzangu karibu ndani.

 

Rafiki wa Esha

Ah! Mi siingii ndani nakaa hapa hapa.

 

Shulea

Inamaana hautaki kumwona Mama?

 

Rafiki wa Esha

Hamna sina maana hio. Napumzika halafu tutaenda. Ndo nimefika siwezi kuondoka bila kumwona mama.

 

Shulea

(Akimpa kiti alichokalia na yeye anaingia ndani kuchukua kiti kingine na kukaa.)

 

 

 

Rafiki wa Esha

(Akimuangalia usoni Shulea.)

Haya habari za hapa na vipi Esha umewasiliana naye?

 

Shulea

Za hapa ndo hivyo hivyo. Mama bado na huyo dada yangu Esha hata simwelewi si wa simu wala sio wa kutuma barua. Nipo mwenyewe.

 

Rafiki wa Esha

(Akiguna.)

Mimi nimemwambia Rafiki yangu Esha kule alipokuwa anapotaka kazi wana roho mbaya. Hata kama anapata hela na mshara wake. Hawezi kutoka nakuzileta huko. Atabanwa mpaka basi.

 

Shulea

(Akistuka na kumtolea macho.)

Ina maana unapajua anapofanyia kazi Esha?

 

Rafiki wa Esha

(Akioneana anaweza kidogo.)

 

Shulea

(Akisimama kwa hasira.)

Mimi naangaika kumbe wewe unapajua. Na sema hivi hatutaelewana mpaka utakaponipeleka huko.

 

Rafiki wa Esha

(Akiinuka kwenye kiti huko anatabasamu.)

Sina maana napajua ila siunajua ukifanya kazi kwa wabongo kupata mapumziko ni kazi sana. (Akimshika mkono Shulea na kuingia ndani.)

 

 

Scene 23

Esha akionekana jikoni anaandaa chakula. Na sahani moja akiweka sumu. Huko sebureni Chidi amekaa na mwanaye na Ally wanaongea.

 

Esha

(Akiwa na wasiwasi na usoni alivyojaa huruma na kuweka sumu kwenye chakula. Kisha anatoka na kuelekea chumbani kwake kwa hasira.)

 

Chidi

(Akimwangalia Ally usoni. Hivi mpango wa kula unakwaje?)

 

Ally

(Akiguna.)

Halafu hata sijua maana Fransi mwenyewe sidhani hata kama kaandaa nimemwona kama katoka.

Rama

(Akiinuka kwa shauku.)

Jamani leo nataka kila kitu niandae mimi. Nataka baba afurahie chakula nilichoandaa mimi ili ajue mwanaye amekuwa mkubwa.

 

Chidi

Hebu acha naye mambo ya jikoni. Hebu kamwite Esha afanye hivyo.

 

Rama

Baba, nimeamua kuandaa kwa hiyo naandaa. (Akielekea jikoni na kuchukua chakula.)

 

Esha

(Akiwa chumbani kwake anafuta machozi na kuinika na kuelekea jikoni.)

Haiwezekani siwezi kuua ngoja nikamwage kile chakula.

 

Chidi

(Akimwangalia Rama usoni.)

We mtoto mbishi. Haya nakula chakula ulichoandaa.

 

Ally

Hamna kaka. Siku moja moja sio mbaya akiandaa.

 

Esha

(Anaonekana kuchanganikiwa alipofika jikoni nakuona vyakula vyote hamna. Anaenda sebureni na anawakuta wanakula. Anastuka.)

Dah! Mmetenga mwenyewe samahani boss.

 

Chidi

(Akiwa na tabasamu huko akimwangalia Esha usoni.)

Bila ya samahani Rama ameamua kujitolea kukusaidia.

 

Wote

Wanacheka. (Ghafla Chidi anaanguka na kutoka povu mdomoni.)

 

Ally

(Akitoa macho na kumwangalia Chidi.)

Kaka una nini? (Akilia na kuchanganikiwa.)

 

Rama

(Akilia.)

 

Ally

(Akimwangalia Esha usoni.)

Esha, njoo tuminue tukamingize kwenye gari twende hospitali.

 

Wakionekana wakimwingiza kwenye gari Chidi na kuelekea hospitali.

 

 

Intercut

Wanaonekana nyumbani huko watu wakijaa msibani na kilio kinaendelea. Mara polisi wanafika msibani na kumkamata Rama kwa tuhuma za mauwaji ya baba yake.

 

Esha

(Akionekana akiwa na uchungu na kujisikia vibaya kwa Rama kukamatwa bila ya hatia.)

 

 

Intercut

Watu wanaonekana makuburini wakionekana kumalizia kufukia. Kisha wanatawanyika Esha anakosa nguvu na kushikiliwa na majirani.

 

 

Scene 24

Esha akiingia chumbani kwa marehemu Chidi na kuiona picha ya mama yake. Anaamua kuitungua juu nakuichukua na anaipeleka kwenye chumaba chake na anaiweka kwenye begi lake. Kisha anaenda sebureni anamkuta Ally na watu wengine wanandugu wakiongea kuhusu kifo cha Chidi.

 

Ndugu 1

(Akimsangalia Esha.)

Ehe. Hebu kaa hapa Esha.

 

Esha

(Anakaa kwenye kiti.)

 

Ndugu 1

Sasa inakuwaje kuhusu wewe? Boss wako ndo hivyo na kama unavyoona na Rama hatujui tutafanyaje.

 

Esha

Mimi nahitaji kurudi nyumbani kwanza.

 

Wote

Wanaangaliana

 

Ndugu 2

Sawa tumpeni luksa kwanza arudi kwao au mnasemaje?

 

Ndugu wote

Sawa kesho aende.

 

 


 

Scene 25

 

Nyumbani kwa kina Esha mchana

Anaonekana Shulea akiwa kakaa nje. Mama yake akiwa kakaa sebureni akiugulia. Mara Esha anatokea akiwa ameshika picha mkononi mwenye furaha na kujiona mshindi wa maisha ya mamake. Mara anafika kwao na kufungua geti. Anakutana na Shulea uso kwa uso.

 

Shulea

(Macho yanamtoka kwa mshangao.)

Esha!

 

Esha

(Akiwa na sura ya furaha.)

Bila ya kuwanza kuongea chochote kwanza mama yuko wapi?

 

Shulea

(Akiguna.)

Ingia yuko hapa sebureni.

 

Esha

(Akionekana akiingia ndani na picha yake. Kisha anakaa karibu na Mamake na kumwamsha.)

Mama! Mama! Mama! Maaaaama!

 

Mama Esha

(Akigeukia upande wa pili.)

 

Esha

(Akiwa kashika picha.)

Mama nimekuwa mshindi wa matatizo yako. (Mara Shulea anaingia na kusimama pembeni.)

 

Mama Esha

(Akionekana kujiinua kwa kasi na kurudi chini na kukata roho.)

 

Shulea

(Akimsogela mama yake huko macho yanamtoka kwa mshangao na kumwinua.)

Mama Vipi?

 

Esha

(Akishangaa na kumshika mama yake anagundua kashakufa. Anastuka na kuanza kupiga kelele machozi yakimtoka.)

 

The End