04/06/12

Ripoti ya WATOTO TALENT SHOW

Tarehe 02/06/2012

 

Ya kwanza niwape shukrani kwa wote ambao walijituma, walioangaika na waliojichosha kwa ajili ya kuwezesha tukio letu la WATOTO TALENT SHOO. Mimi nimefurahi sana niliona watoto walikuwa wenye furaha na nashukuru kwamba bado kila kitu kiko kizima.


Pia Toni alitufurahisha na show yake ya mazingaumbwe. Nadhani hilo siku wote walipata hisia ya sherehe. Ua ulikuwa safi na ulipendeza, tulipamba vizuri na watu walifurahi kuona hivyo. Nilisifiwa na watu wengi japokuwa naona kuna mapungufu mengi sana kutokana na kuchelewa kuanza maandalizi.


Ya kwanza wageni waalikwa wengi hawakufika. Bahati nzuri majirani wengi walifika kwani uani kulijaa watu na watoto wengi. Wengi kati watu wangu hawakufika kwa sababu sikuwakumbusha tena na voluntia wengi wanasafiri sasa hivi. Ningewasumbua kwa kuwapigia simu wangekumbuka na labda wengine wangekuja.


Namshukuru Hamis kuwafuata wakubwa ili tulikuwa na wageni rasmi kama Mama Natasha waliokabizi washindi zawadi zao. Hata Josephat alichelewa sana.

Na pia BABA WATOTO walichelewa sana kwa sababu hawakupigiwa simu tena. Kwa hiyo walishiriki nusu tu. Wangeweza kushinda wangewahi. Walilalamika kwamba hatukuwaambia muda wa kuanzia. Lakini walipokea barua mapema. Labda taarifa haijafika kwa sababu Mkude hayupo, kasafiri.


Pia majaji walichelewa na wengine hawakujaji kabisa mpaka walibuni kwenye maigizo kwa sababu waigizaji hawakuwepo. Mara ijajo itabidi tuhakikishe kwamba waje kweli na kutokuchelewa halafu tuwaeleze vizuri wajaji vitu gani.


Na pia kamera ilichelewa lakini sio vibaya sana. Hamisi alijitahidi na badaye tulikuwa na kamera tatu. Pia alikwepo mwandishi wa habari aliyefanya interview na waalimu. Kwa hiyo WATOTO TALENT SHOO itaonekana hata kwenye TV na gazeti na itasikika kwenye redio.

Sasa nina swali kwenda studio: Je, mtaedit ile video na itakuwa filamu au klipu nzuri? Maanake Toni aliniomba awe nayo. Lakini sasa zile hela zimepotea. Mtafanya kazi hata hivyo?


Pia kapeti jukwaani haikupatikana na watoto waliigiza na walicheza chini wakati jukwaa lipo. Ingependeza wangeweza kupanda jukwaani hata kama kuna nafasi ndogo tu. Kwa nini hawakupanda katika maigizo? Lakini mara nyingine inabidi tuwe na kapeti.


Mkurugenzi na mimi tutaandaa Maombi kwa Bernhard Staub baada ya muda sio mrefu sana. Na tuangalie kama inapatikana.

Kwa ajili ya kucheza chini na kutokana na jua viti vya adhira vilipangiliwa vibaya na nyuma sana. Sikupenda wageni walivyobanana na walivyokaa mbali ya jukwaa. Siku nyingine tupate kimvuli au tutakuwepo sehemu nyingine kabisa?

Halafu sio vizuri kuwaambia watu kwamba watapanda wasanii wakubwa halafu hawapo. Angalau Uyoga Boga Village walipafom japokuwa sikuwaona. Band ya Oliver wangeweza kupanda au tungewauliza wengine, lakini nadhani hatukuwauliza. Maanake mara nyingine tuanze mapema kuwatafuta.

Tuseme hata wiki hii tunaweza tukaanza maandalizi ya WATOTO TALENT NUMBER TWO!


Tujiandae vizuri ili tuwe na utaratibu. Sijui kama nilikiona mimi peke yangu au saa nyingine haikueleweka nani yupo na tukio gani lipo kwenye mashindano. Hata majaji walichanganikiwa. Tulishindwa kuwaelekeza vizuri kabla ya shoo haijaanza.


Hapo ndo nimsifie Kayombo. Katika kuchagua mshindi alimiliki vizuri. Hata kama amekosea kuandika kwenye vyeti. Mara nyingine lakini itabidi tuwe na printer yetu ofisini. Bahati mbaya iligoma siku ya shoo.


Halafu TSE ilishinda sana yenyewe. Naogopa kwamba washiriki wengine hawapendi kuja kwenye WATOTO TALENT ijaoyo. Tuwape mashariti ya kujaji mapema ili waweze kujiandaa vizuri. Hivyo watalalamika haki hazikuwa sawa kwa kila kikundi walichoshiriki. TSE tulijua mashariti mapema na mazima. Tuwe na utaratibu mzuri tusijichanganye, wote waelewe kila kitu.

Halafu mziki ulikuwa mbaya. Hata tungeweza kutumia spika zetu na mziki ungelia vile. Mara nyingine tupate viombo vya Live Band.

Kutukana na ule mziki mbaya hela zingine zilibaki. Zile tuligawa kuwalipia wahusika nauli.


Halafu kusikitika ni kwamba wageni hawakununua hata kitu. Labda wangenunua tungetangaza zaidi? MC peke yake aliongea tu. Sijui kama watu walimsikiliza muda wote. Mara nyingine nashauri apande mhusika wa kalcha/ uchoraji/ albam na zile bidhaa nyingine. Apande jukwaani kabisa na aeleze vizuri ili inavuta kununua. Na ushonaji vipi? Kwa nini sikuona mishono jukwaani? Tungeweza kuuza kama wageni wangeangalia zaidi lakini sukuwaona wakiangalia.

Nadhani vitu muhimu nimevitaja sasa. Tukae kikao mapema tujadili tulichojifunza kitu gani na tuanze kuandaa WATOTO TALENT NUMBER TWO!

Cha kufanya ni:

  • Kupanga tarehe (11/08/2012?)
  • Kuanza kutangaza/ Tusumbue watu ili wasisahau/ Internet na Facebook
  • Tuandae maombi ya kuwatumia KAWAIDA mapema
  • Tukae Kikao wiki hii!

Lakini malengo ya WATOTO TALENT SHOW tuliyafikia. Watoto waliongeza juhudi, walifanya mazoezi mazuri, hata mara kwa mara walikuja nyumbani kwetu kufanya mazoezi ya dance baada ya TSE usiku. Watu wengi walifika TSE na walifurahi waliona TSE na inazidi kujulikana.


Natumaini ripoti hii itatusaidia.


Asante tuko pamoja. Na tunaweza kushiriki na kushinda.

 

Franziska