Ubungo/ DSM; 22/01/2012

Ripoti ya TSE (Franziska)

 

Naandika ripoti hii kwa ajili ya kujifunza na kuwafundisha walimu wa TSE. Wapate tathimini yangu na wajifunze mambo yangu. Kitu hiki ni muhimu kwa sababu (bahati mbaya) nipo hapa kwa muda mfupi tu. Ni lazima wanijulishe haraka kwa hiyo wasome ripoti hii kwa uangalifu.

Sasa hivi nimefanya kazi TSE kwa muda mrefu. Nimewazoea watoto na walimu wenzangu. Nawapenda sana na pia nafikiri wananipenda pia ila sina hakika kwani hawajaniambia.

TSE na kazi yake naipenda sana kwa ujumla. Naona ni sehemu nzuri sana kwa watoto. Wanaweza kujifunza vitu vingi ambavyo vitawasaidia katika wakati ujao. Na sasa hivi wana nafasi ya kukutana na wenzao na kufanya vitu vizuri pamoja.

Na walimu wanajitahidi sana kwa sababu wanafanya kazi vizuri hata kama kuna tatizo la umeme na vifaa. Bado TSE ni kituo kidogo sana lakini kimeshafanikiwa vitu vikubwa na pia naona kinasonga mbele. Mwaka uliopita tumepata vitu vingi sana vinavyosaidia katika mazoezi ila ofisi imejaa. Lakini sasa kuna mpango wa kuhamia sehemu tofauti mwaka unaofuata. Halafu kuna mawazo mazuri na miradi mipya kama tamthilia na kutengeneza kalcha!

Kwanza mradi wa kalcha unaendelea hakuna shida ila sijui kama utaendelea vizuri kama sasa katika wakati ujao. Labda watoto watachoka? Lakini Madamu Haika ana nia nzuri ya kuendeleza mradi huo. Anataka kufundishwa kila kitu, ataokoa mradi huu wakati ujao nikishaondoka!

Tamthilia ni mradi mzuri lakini ni mkubwa sana! Kituo kidogo kama TSE hakiwezi kufanyikia mradi mkubwa kama ilivyopangwa mwanzoni. Sasa tumekubaliana kuanza na episode ya kwanza na mazoezi ya episode zinazofuata. Na pia hatujui lini tutapata fedha za kuanza kurekodi. Kwa hiyo kufanya mazoezi kwanza si vibaya hata kidogo! Tufanye taratibu kwa sababu harakaharaka haina baraka! Kuna kitu kimoja tu ninachoogopa, kwamba watoto wanakuja na kuondoka TSE kwa hiyo itakuaje kwenye tamthilia?

 

Hivyo basi ninafikiri kwamba.

Sijui bado walimu na watoto wanaonaje kazi yangu. Nafanya kazi vizuri au kuna kitu fulani ambacho nakikosea au tabia yangu inawasumbua? Sijaambiwa bado; sipati tathimini ya kazi yangu hata kama nimeshawauliza. Je, mmeridhika kwa kila kitu au kuna mapungufu yoyote? Kama kuna mapungufu naomba mnijulishe tafathali.

Kwa mfano kama nachelewa ofisini najisikia vibaya hata kama nimeshamwambia Madamu Haika na ameshakubali. Mara kwa mara nafanya kazi nyumbani, kama kuandika barua, maombi, risiti, kuandaa mazoezi nk.. Kwa sasa nafanya hivyo wikendi, usiku au asubuhi. Nachoka! Lakini kama najaribu kufanya hivyo asubuhi ofisini, hata kama sina kazi nyingine, navurugwa na wakina Rama au naanza kazi nyingine. Ningeweza kuandaa mazoezi ya sarakasi ningewafundisha watoto vizuri zaidi.

Halafu „weltwärts“ inaruhusu masaa manane kwa kila siku tu. Naanza kazi saa mbili au saa tatu asubuhi hadi saa kumi na mbili au mara nyingi zaidi. Wakati mwingine tunakaa kikao baada ya TSE au wikendi na halafu nina kazi za nyumbani. Nayapita masaa manane ambayo yameruhusiwa.

Si tatizo kwangu kufanya kazi zaidi kwa sababu naipenda ila nachoka. Na pia ningependa kuzunguka zaidi, kuona sehemu mbalimbali za Dar es Salaam na kutembelea marafiki. Na pia sipendi kujisikia vibaya nikichelewa ofisini. Labda kuchelewa ni kawaida tu kwa sababu naona walimu wengine wanachelewa pia. Kwa Ujerumani nimezoea kuwahi kwa hiyo ninajisikia vibaya.

Kwenye semina ya jana mkurugenzi Alfred ameongelea hivyo pia. Alisema sisi voluntia tupo hapa kwa ajili ya kujifunza utamaduni na tusione sehemu ya kufanya kazi tu na pia tupate muda wa kupumzika.

Kwa hiyo ingekuwa ni tatizo ningetoa taarifa “Leo asubuhi siendi TSE niandae mazoezi ya sarakasi peke yangu na nyumbani.”?

 

Swala lingine ni kwamba naogopa kukosea mbele ya Mkurugenzi Alfred. Sipendi kama anakasirika kwa ajili ya mimi. Anajua lakini kwamba bado najifunza. Naona ananisamehea na hanichukii. Kama nimekosea mniambie! Nimetaka kutamka mabo haya mara moja kwa sababu kitu cha muhimu.

 

Halafu nina pendekezo lingine. Tuunganishe kazi za walimu zaidi. Muziki, maigizo, kuimba na ngoma zinashirikiana tayari lakini kwa upande wangu bado. Napenda kushirikiana zaidi pamoja na kazi za walimu wengine. Kwa ajili ya haya tukae kikao siku moja tujadiliane! Na pia Teacher Mors ameshaniambia anataka kushirikiana na mimi na programu ya kuchora.

Kama nimewakosea naomba mnisamehe na mniambie. Natumaini ripoti hii mmeelewa na itawasaidia!

 

Franziska Müller, voluntia wa TSE