Mradi  wa  kuchora

(kwa kiswahili)

 

Picha zake za mradi wa kuchora nimeshaaplodi muda. (Kuangalia picha bonyeza hapa.) Sasa ndo inafuata ripoti yake japokuwa muda umepita tayari kidogo.

Kila kitu kimeanza na hamu yangu ya kuanzisha mradi mdogo mpya huko TSE. Kwani mziki unafundishwa sana, mafunzo yangu ya sarakasi yamekuwa magumu kidogo na kwa sababu mimi mwenyewe nimependa kuchezea rangi, nimeamua kuanzisha mradi wa kuchora. Pamoja na Mors mwalimu wa Hip hop tumewaandikia ombi la mradi KAWAIDA. Tukishapata fedha tulienda mjini kununua vitambaa, rangi, brush, mbao, vinyundo, misumeno na misumali. Chogo ambaye ni mchoraji mwenyewe na anayejua kuchora sasa hivi alinisaidia sana. Tumekubaliana kwamba mimi namsaidia kuuza postkadi zake ujerumani na yeye ananisaidia mimi kuwafundisha watoto wa TSE kila jumatano ya pili.

Jumatano ya kwanza tulianza kukata mbao ma kugonga msumali kwenye frem za kuchorea. Watoto walikuwa na changamoto na walipenda kumsikiliza Chogo na umakini akiwaelezea kitu.

Asubuhi siku zingine nawatolea watoto rangi na karatasi kwa ajili ya kufanya mazoezi ya kuchora na kubuni picha abazo zichorwe kwenye frem badaye. Kufikia sasa nimeshasanya rundo kubwa la picha za mazoezi.

Mwanzoni kila kitu kimeenda taratibu sana… Baada ya wiki mbili jumatano moja tu tulikuwa na kipindi cha kuchora na kama haijafanyika mara moja tulisuburi hadi wiki nne. Hivyo tuliendelea mpaka frem zilikuwa na mashikizo kwenye mapembe, zilivalishwa vitambaa na zingine zilipakwa kozi ya kwanza. Halafu Madam Haika alilalamika kwamba ofisi imejaa vitu vingi na frem zinazuia. Yeye katoa wazo la kuchora kila kipindi cha mazoezi katika wiki nzima. Baada ya hapo tuliamua kukaa kikao na mkurugenzi. Katika kikao hicho niliweza kupanga wiki moja kwa ajila ya uchoraji peke yake.

Lakini katika kikao hicho tulimuongelea na Chogo. Chogo anakataa kumwamkia mkurugenzi. Tabia hizo Alfred haipendi kabisa. Hata mara nyingine Chogo hapendi kuwatii watu lakini ananisaidia sana na anapenda kufundisha uchoraji. Lakini Alfred kaamua Chogo asije tena kufundisha mpaka amletee barua ya msamaa kwa sababu anawafundisha watoto tabia mbaya. Mors amemtolea taarifa Chogo. Chogo kasikitika lakini hajaandika ile barua. Katika ile wiki moja ya kuchora ningemhitaji Chogo wa kunisaidia, lakini hivyo hakuweza kuja tena…

Wiki hio imeshapita siku nyingi lakini hata hivyo nataka kuwaelezea tena:

Jumatatu nilifika TSE na dumu empty na nilivyolikata vipande vipande tulipata sahani fulani kuchanganya rangi.

Waalimu wengine hawajaweza kunisaidia sana katika kuchora. Wengi walichelewa kwa sababu nilivichukua vipindi vyao vyote lakini baada ya muda wote walifika kwa sababu walidadisi uchoraji. Lakini mimi peke yangu nilikuwa na makukumu kuwafundisha watoto wengi, na kulinda rangi, brush na frem. Kiukweli niliogopa kidogo kwamba kitaharibika kitu.

Nilianza kwa njia kuwaelekeza jinsi ya kuchanganya rangi na kushika brush. Halafu ndo tumeanza!

Nimependa kuwaona watoto walioanza kuchora kwa namna nyingi tofauti. Ilikuwa mara ya kwanza kushika brush ya kuchorea mkononi. Wengine walijua kuanzia mwanzo watachora nini, wengine walianza tu bila kufikiria na wengine walipata wazo taratibutaratibu. Lakini hata mtoto moja hakuogopa kupaka rangi au kwamba anaweza akachafua kitu.

Wengine waliniuliza maswali kibao na niliangaishwa, wengine walikaa kimya na walichora bila kunidai mashauri. Sikutaka kuwaagizia chochote na kuona zitatokea nini. Kama waliniita niliwasaidia na kama niliona kwamba anakosea nilimwambia.

Kuanzia jumanne tulianza kuchora kuanzia asubuhi. Watoto walifika mapema ili waweze kuchora siku nzima. Halafu sio tatizo kwa sababu kuchora haina kelele inayowasumbua majirani.

Ilikuwa imenichosha kidogo kwamba niwepo siku nzima, wanafunzi waweze kuniuliza na nilipaswa kuviangalia vifaa visiharibike na visipotee.

Kwa nini hawawezi kuweka brush mezani au kwenye kikopo cha maji baada ya kutumia badala ya kutupa chini kwenye mchanga? Kwa nini wako wazito kufunga chupa za rangi baada ya kutia rangi? Na kwa nini wote wagombanie brush moja wakati zipo nyingi kutosha kwa wote? Majukumu yangu yalikuwa kuhakikisha taratibu na kulinda vifaa.

Lakini yapokuwa na fujo zimetokelezea picha nzuri sana.

Kwani niliamua mwanzoni kutokuwaambia watoto vitu vingi na kuwaacha wachore wenyewe, hawajanisikiliza sana nikiwaambia kitu. Wengine waliharibu picha zao hata kama niliwahi kuwaambia wasiendelee tena picha inapendeza tayari wasipake hata rangi tena. Lakini nilisikitika wengine walipakia rangi tena kote na kuanza tena upya.

Ijapo yoyote nilifurahia mradi huu sana kwa sababu ya motisho na uchangamfu wa watoto.

Ilivyo tulikuwa na picha nyingi halafu nzuri sana kwa ajili ya kuonyesha katika tamasha letu la WATOTO TALENT SHOW. Lakini nilistuka kwamba wazazi wachache sana tu waliwahi kuangalia picha ya mtoto wao.

Pia kwa ajili ya show nilitengeneza bango lililobandikwa nyuma ya jukwaa na lilionekana katika maonyesho.

Sijajuwa kabisa mradi wa kuchora utaendeleaje lakini kama naombwa rangi, brush au mashauri na mtoto yayote nampa. Tena nitanunua mbao wa kutengeneza frem mpya na kitambaa cha kuvalisha. Lakini sina uhakika kama wataendeleza changamoto chao. Nitamfundisha Roger kuwafundisha uchoraji na wadogo kwa sabababu yeye anakumbuka vizuri na labda anaweza kuendeleza mradi huo wakati mimi nikishaondoka. Nitakaa naye vizuri na kumelekeza.

 

Franziska