Tarehe 30/10/2011

Ripoti ya kwanza baada ya miezi mitatu

 

 

Sitaki kuamini kwamba sasa robo ya muda wangu ambao nimeishi hapa Tanzania umeshapita. Muda unapita haraka sana kwani vitu vyingi vinanitokea kila siku. Hakuna kuchoshwa, kila dakika kuna vitu ambavyo ninavifanya, ninaviona au vitu ambavyo nataka kuvisoma.

Taratibu naona ovyo ovyo kichwani mwangu inazingua. Sasa sioni vitu na watu tu lakini naanza kuelewa. Ya kwanza nimeona Tanzania na watu wote kama shaghalabaghala lakini sasa najua sio kama hivyo.

Kwenye ripoti hii nataka kujaribu kuelezea ili ile shaghalabaghala imezingua (au bado) hadi imewezekana na pia nataka kuonyesha vitu ambavyo naviona kwa macho yangu, vitu ambavyo nasoma hapa na vitu navyofanya kila siku.

 

Siku ya kwanza nilishangaa tu. Nimeona watu wakitembea haraka wakipiga kelele lakini wote tumekutana wema na furaha. Mnasalimiana hata msipojuana.

Pia nemeona kitambaa cha rangirangi na matunda mengi. Barabara ambazo zimejaa magari mengi, kelele, takataka na mawe kwenye njia. Nilifikiri kila hatua niangalie sakafu ili nisikwae jiwe. Nilikuwa nahisi tu siwezi kujua niende wapi na kuona chochote kinachonizunguka. Nimezidiwa kwa vitu vyingi. Lakini nilifurahi kila wakati kwa sababu ya habari nyingi na nzuri! Taratibu nazoea kuishi Tanzania.

Ndio kama kwenye njia ya mawe sasa naweza kuangalia sehemu nyingine ila kuangalia sakafu tu. Nimezoea kutembea na kuona mawe njiani.Kama hivi nina vitu vyote: Baadaye nilizoea kitu kimoja au baadaye nimeelewa kitu kimoja naweza kuona vitu fulani vingine. Kuna vitu ambavyo napita kila siku lakini sijaviona kwa kweli kwasababu nimefikilia kitu kingine kwahiyo sijaweza kufikiri kitu hiki. Wakati huu naanza kuelewa watu ambao wamenizunguka.

 

Vilevile na lugha. Kwanza nilisikia toni tu na sasa naweza kuelewa kidogo au angalau kusikia maneno yanayoanza na yanayomalizia. Inategemea naongea na nani na sauti za watu kuzizoea hata sijaelewa maneno yote. Baada ya muda mfupi nelijua kusema kwa kuomba kitu fulani au kuwauliza watu. Sasa naelewa hata majibu mengi.

Naanza kuzungumza kidogo na kujulishana vitu tofauti tofauti na watu kwa muda mfupi naweza kuongea na wenzangu na kujulishana mambo wanayoyapenda, wanaishi maishi yapi, vitu ambavyo wanafikilia na wanavifanya siku zote. Nafurahia kujifunza kiswahili na nafulahia kuongea na watanzania pia. Hata nafikiri pia wao wanapenda kuongea na mimi. Wengi wanajitahidi kunieleza maneo ambao siyaelewi.

 

Muda mwingi nimesemeshwa na watu ambao sijawahi kuwaona hata kidogo. Ndio labda kwa sababu wanafurahi kuongea na mzungu. Mara nyingi inachokesha kusalimiwa kwa pande zote (mara nyingi kwa kiingereza). Pia wananiita Mzungu! Mitaani mara nyingi. Sijui kwa sababu gani wanafaya hivyo. Hata wale wenyewe ambao wananiita wanafahamu sio tabia nzuri.

 

Mimi sijui sababu ila napendelea kama wananiita jina langu ambalo nasikia zaidi sana. Mimi nimejulikana sasa. Ningesalimia watu wote njiani wakati nakwenda kazini ningehitaji saa nzima hadi kufika ofisi ya TSE. Hata nimeshaalikwa nyumbani kwa watu kwenye njia kwenda kazini imeshatokea hivyo zaidi ya mara mbili. Ghafla nilikaa kitandaani bado kidogo nimenuliwa soda au nimepikiwa chakula. Kabla ya kazi asubuhi! Mwaliko nimeusogeza mpaka jioni lakini hata hivyo nimechelewa kazini.

 

Vipindi kama hivyo vinatokea ghafla (pia sikukuu). Kwa mfano tokea jana naigiza kwenya filamu ya bongo. Rafiki yake na mtu wa kujitoleo wa zamahani ni mchezaji wa filamu. Kwa filamu hii wanahitaji bado wazungu sijaulizwa sana lakini kwa sababu nimependa wazo hili na nimekubali kuangalia kazi zake. Mpaka sasa sijui vizuri mambo ya filamu. Lakini jana nimeuwawa na mazombi (vampires).

Zile filamu za bongo zinatengenezwa katika muda mfupi sana na kwahiyo zinatokea vibaya. Watengenezaji wanahitaji wapewe hela tu, sio vitu vyingine. Muda mwingi nimepata hisia hela peke yake inatoa sababu kwa kazi zao. Wote wameonekana hawapendi kazi zao. Wanafanya kazi mpaka wapewe pesa ya kutosha na sio zaidi kama sio lazima. Sio vizuri kusema hivyo kwa wote lakini jambo hili linahusu. Nafikiri hakuna mtu ameandika mswada au anajua mabo ya filamu. Inaonekana kama watu wote wamealikwa ila wameelekezwa mambo ya filamu. Hata tumeanza kushoot filamu bila vifaa na nguo kwa ajili ya filamu. Walizema nguo zinawezakana kubadilishwa kwa kompyuta baadaye. Pia kufuta makelele ya kaniza lililokuwa pembeni.

 

Sababu moja peke yake ndio mtengenezaji kupewa hela. Yule mchezaji mwenyewe alisema haangalii filamu kama hio kwa sababu ameiona mbaya. Lakini tumefurahi kushirikiana kwenye filamu na nataka kuoana matokeo ya filamu hio.

 

Sasa nataka kuznumgumza kuhusu TSE (Talent Search and Empowerment), mradi wangu. Hii ndio kama nyumba ya watoto na vijana ambao umri wao ni kati ya mwaka moja hadi miaka 20 na wakubwa wachache wanafundishwa kompyuta wanahudhuria hapa TSE. Watoto wanaofundishwa bure na wakubwa wanalipa ada lakini wote wajaze form.

 

Nilipoona sehemu ya kazi yangu mpya kwa mara ya kwanza nilishangaa kwa sababu TSE ni jengo moja dogo na vyumba viwili vidogo – darasa la kompyuta na ofisi – halafu uani (kuna takataka nyingi na vumbi sana) Huko walimu wanafundishia sanaa.

 

Wenzangu wana miaka mingi zaidi ya mimi lakini sio sana ila Madamu ambaye anafundisha kompyuta na pia ni karani (secretary). Walimu wengine wanafundisha ngoma, Hip Hop, maigizo, kucheza mpira wa miguu. Mimi nilifika hapa na wazo la kufundisha sarakasi.

Lakini mpaka sasa sijafundisha sarakasi sana. Idjumaa ni siku yangu ya kufundisha sarakasi lakini wiki tano zilizopita ilikuwepo mradi wa maigizo na wiki kabla imetokea sikukuu (ghafla). Mafunzo yanafuata (ila mafunzo la kompyuta) mchana au jioni kwa sababu asubuhi jua kali sana na watoto wengi wanafika mchana. Mimi nipo kutwa mzima, nafika saa mbili au saa tatu na natoka saa kumi na mbili jioni.

 

Sasa hivi nafanya vitu vyoyvote tofauti tofauti na kwanza kabisa sijakuwa na kazi muda mwingi nilikaa uani ili kuangalia aukuongea na walimu. Sasa namsaidia Haika kufundisha kompyuter umeme ukiwepo. Siku moja umeme haupo nikicheza mchezo ya mdogo na wakubwa kwa sababu watoto walishakimbia. (Muda mwingine nafikiri hata wakubwa wanapenda kuwa wadogo.)

Pia nafundisha kusuka kalcha, nasafisha ofisi (kila mara nashangaa uchafu mwinigi unatoka wapi.), nachora picha au naangalia watoto ambao wanapenda kufanya utundu. Bahati mabaya kwenye kontena kutoka ujerumani zilikuemo rangi za maji na kitabu na picha za watoto wanapakwa nyuso rangi. Kwahiyo ilikuwa kazi sana kuwaelekeza wasipake nyuso lakini wachore kwenye karatasi.

 

Pia nafundisha watoto kutembea kwenye kamba, napeleka hela kutoka upande mwingine wa DSM, nafanya mahesabu ya ofisi, naandika vitu tofauti kwenye kompyuta natafsiri ripoti za walimu kwa kiingereza nakuzituma kwenda ujerumani, nasaidia kuonganisha safari za kwenda baharini kila mwezi nauza viniwaji, nafundisha mahesabu, Kijerumani na kuandika (lakini sio kama shuleni, nafundisha mtoto mmoja au wawili tu na muda mwinigi bila mahusiana.

 

Kila dakika niko bizi na kitu chochote. Mara nyingine nimetumwa kazi moja kwenda nyingine. Mara nyingi nasitishwa. Vitu vyote vinaenda bila coordination na watoto hawana usikuvu. Nikifanya kitu kidogo kingine wanakimbia katikati ya kazi na wanaendelea na kitu kingine ingawa kwanza walipenda kufanya ninachofundisha. Muda mwengine na fagia uani hakuna mtu hasipotaki kufanya hivyo, nafundishwa gita kidogo, nawapeleka masalani watoto wadogo, natafuta kalamu sana nk…

 

Nimeaminiwa na nimepewa madaraka sana labda zaida ya naweza kushinda. Kwanza sijaona hivyo. Nilifikiri hapa kuna ovyo ovyo tu na kwa ajabu hakuna kitu kilichovunjwa.

Sijasikia kuna madaraka lakini nilipewa madaraka ya kazi hapa. Mimi ambaye nimetoka shuleni na sijui hata kidogo watu wa hapa wananiamini, wanafiri mimi ni mkweli. Kazi yangu ni kuleta kipaji cha Dogodogo-Center ya zamani, ndio nyumba ya yatima ambayo imefungwa. Kipaji sasa TSE imepewa, kama kuna kosa litakuwa kosa yangu kwa hakika lakini naona wote wananiamini.

 

Sipendi kwamba mzungu anfanya mambo ya hela ya kituo cha Tanzania. Sio sahihi kama mgeni anafanya hivyo na kwa sababau tu ambaye ameaminiwa. Ya kwanza ni mchuuko (stereotype) kwamba mzungu analeta pesa na ameona kama mkweli na pili itakuwa vizuri kama watanzani wangeweza wenyewe. Angalau mshahara wa walimu wa TSE kutoka “Kawaida” imetumwa kwenye akaunti ya mkurugenzi Alfred kwahiyo sihitaji zaidi kulipia watu.

 

Kila jioni nafurahi kuwa kimya lakini mara nyingi watu fulani wanatutembelea kwa sababu wanataka kutusalimia. Watu wanapenda kuishi pamoja. Kila wakati wanakaa au wanatembea nje kwenje mitaa, nyumbani wanakaa muda mfupi tu. Inafana na campsite ya unjerumani huko tunapika mswaki mbele ya hema. Kuwa mwenyewe inachokesha. Neno “peke yangu” pamoja na maneno kama “upweke” na “uzuni” nimefundishwa pamoja. Napenda kuwa na watu wengi lakini nafurahi kulala peke yangu kwenye kitanda changu.

 

Kwa kuwa hapa na napenda sana nafurahi sana. Sipendi muda unaenda haraka kama sasa. Mara nyingine ni ngumu sana lakini ni vizuri. Nina kazi nyingi, mara nyingi nimetaabishwa lakini ni zaidi kama nisingejua nafanya nini na muda wangu.

 

Sasa nimewaambia vitu vyingi lakini sijaambia vyote lakini haiwezekani kwa sabuabu vitu vyingi vinatokea kila wakati na pia tunaviona.

 

 

Dar es Salaam /Tanzania

Franziska Müller, voluntea wa “Kawaida e. V.“