Franziska Müller aka Fransiska Maleko

Ninaitwa Franziska Müller

 

Nina miaka 20 na tangu mwezi wa nane mwanzoni naishi Dar es Salaam na nafanya kazi kwenye kituo kidogo cha watoto kinachoitwa TSE.

 

 

Nafanya nini huko Tanzania?

 

Nawafundisha watoto wa TSE sanaa tofauti kama kwa mfano kuchora, kuruka sarakasi na kutembea kwenye kamba. Lengo langu ni kujenga kikundi cha sarakasi hapa Tanzania kwa sababu Ujerumani nimeruka sarakasi sana na naipenda.

 

 

Kwa sababu gani nafanya hivyo?

 

Baada kukaa shuleni miaka 13 nataka kufanya kitu tofauti, nataka kuishi bila wazazi, kufanya kitu cha maana na kujifunza vitu vipya kama utamaduni na maisha ya Tanzania.

 

Kama mnaangalia Blog yangu mtaona!